UNESCO

  MANIFESTO YA JUMUIA YA VIJANA KWA KARNE YA 21.

1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.

Wakiwa wamealikwa na Bunge la Ufaransa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), Bunge la watoto duniani walikutana kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 21hadi 27Oktoba 1999 katika jiji la Paris. Mkutano huo ulihudhuriwa na watoto 350 toka katika nchi 175.

Katika mkesho wa mwaka 2000, mwaka uliotabgazwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka wa kimataifa wa "utamaduni wa amani."Kila kijana alikuwa na shauku ya kutoa fasili yake kuhusu ulinzi wa amani, mshikamano, kuhusu elimu na utamaduni, maendeleo ya kiuchumi na ya kibinadamu na kuhusu kinga ya vyombo vya habari kwa kukubali azimio ya Manifesto ya Jumuia ya vijana kwa karne ya 21 ya tarehe 23 Oktoba 1999.

Manifesto hii inrasimisha izingatio wa vijana wa kanuni ambazo zilizowahi kuhamasishwa na Azimio la haki za binadamu na haki ya raia ya mwaka 1789 na Tamko la kimataifa kuhusu haki za binadamu la tarehe 10 Desemba mwaka 1948.

Manifesto hii ilipelekwa mbele ya ya Mkutano Mkuu wa UNESCO tarehe 26 Oktoba 1999. Ilani hiyo ya kanuni itapewa kwa watala na viongozi wa nchi mbalimbali, vile vile kwa Maspika wa mabunge, na mwanzoni wa mwaka 2000, itatangazwa rasmi kwa Umoja wa Mataifa.

Federico Mayor
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco

Laurent Fabius
Spika wa Bunge la Ufaransa


Maandiko ya Manifesto:

Sisi vijana toka katika nchi 175 tukiungana chini ya mwanvuli wa Bunge la watoto duniani tarehe 27 Oktoba 1999, tuliikubali Mnifesto ifuatayo:

1. AMANI NA KUTOTUMIA NGUVU.

2. ELIMU.

3. VYOMBO VYA HABARI.

4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU.

5. MSHIKAMANO.

6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.


1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.

1.AMANI NA KUTOTUMIA NGUVU.

Sisi vijana wa karne ya 21, tunataka karne hii iwe ya amani miongoni mwa mataifa yote. Staarabu, tamaduni, na dini anuwai duniani zote zina lengo moja tu: kudumisha hali bora ya walimwengu na ulinzi wa amani. Hii ndiyo falsafa ya msingi ambayo mataifa yote yanatakiwa kutangaza. Ni vema kuchanganua yaliyopita ili kupata fundisho katika siku zijazo, lakini ni bora zaidi tujaribu kuondoa mminyano ama ukandamizaji wa wakati huu.

Dunia haina budi kuwania amani kwa njia za kidiplomasia, mazungumzo, juhudi za pamoja na kwa njia zingine zote zile mujarabu. Amani siyo ndoto bali ni lengo la kutimilika. Amani ni kilele ya kufikia, lau kana, Jumuia ya kimataifa itanuia hivyo na kuiendeleza. Kwa dunia nzima ni tumaini pekee ya kuendelea kuishi. Vita ni ugonjwa mbaya sana. Vita vilianzishwa na watawala vipofu, ambao walisahau kwamba kutokana na mipango yao ya kivita, walizima mustakabali wetu na dahari walizika chini ya magofu haki yetu ya kuishi na ya kuwa na siha. Miongoni mwa chanzo za vita viliorodheshwa ni mgao usiokuwa sawa wa mali, chuki zitokanazo na ubaguzi wa rangi, imani za kidini, kiitikadi, na kijinsia; utaifa potofu na ughaibu wa demokrasia na mifumo ya kiutawala ya kiimla.

Kutokana na hali hiyo tunapendekeza yafuatayo:

 


( Kazi hii imetafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha ya Kiesperanto na Mwalimu Matabaro Minani Semutwa mkazi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.)

 enpaøigis : Daniel Durand